Mwaka uliopita, kikundi cha vijana 18 walikutana pamoja kila juma kwa masaa machache kuanza kujaribu "maigizo shirikishi" vipande kuhusu maisha ya Bahá’u’lláh na Báb. Kwa mfano, walitengeneza igizo kuhusu eneo la bustani ya Riḍván, ambapo Bahá’u’lláh alitangaza mbele za watu Ujumbe wake. Katika igizo hilo, watazamaji waliingia katika mahema yaliyojazwa mauaridi, walipewa vikombe vya chai na wakizungukwa na sauti za Nightingale. "Walima bustani" waliingia katika mahema na kusimulia uzoefu waliopata walipokua mbele ya Bahá'u'lláh. Saa hizo, igizo refu shirikishi lilioneshwa ndani ya siku tatu na lilihudhuriwa na watu 180.
Mwaka huu, katika kuadhimisha sherehe za miaka mia mbili,kikundi kiliamua kuandaa igizo na kulionesha kwa watu wengi zaidi. Vijana 30 kutoka vitongoji mbali mbali huko Melbourne walijifunza hadithi pamoja, wakikariri sehemu zao na walifanya mazoezi kwa kina.
Igizo lilioneshwa kwa saa moja na nusu. Watazamaji wake walisindikizwa katika safari kupitia masoko, magereza, bustani, wakishuhudia kila wakati kwa mara ya kwanza. Baada ya kila igizo, watazamaji walialikwa kukaa na kuchunguza maswali kuhusu maeneo tofauti katika igizo na kuhusu Imani ya Kibahá’í pamoja na waigizaji. Moenesho 14 yalihudhuriwa na watu 40 kila moja. Mwisho wake, yaliwafikia watu 560.