Dominika

Jumuia yakusanyika katika kuta zilizopakwa rangi kwa ajili ya maadhamisho ya miaka mbili

Katika visiwa vya Karribien vya Dominika, vijana wa Kibahá’í katika mji mkuu wa Roseau walichora picha za kupaka rangi ukutani katika senta ya Kibahá’í kama zawadi ya sherehe za miaka mia mbili. Jumuia ilikusanyika kandokando ya eneo la ukuta, watu wengi walisaidia kuleta vifaa kama rangi. Jengo hilo lilikua halijapakwa rangi kwa miaka mingi, na vijana walianza kufuta rangi iliyochoka na kuimarisha misingi ya ukuta kwa mawe yaliyokusanywa kutoka baharini. Wiki chache baadae, wakati kimbunga Maria kiliharibu kisiwa chote, watu wengi wa Newton walitafuta hifadhi katika Senta ya Kibahá’í, mojawapo ya majengo machache ambayo yalikuwa bado yamesimama baada ya uharibifu kutokana na kimbunga. Ingawa kulikua na uharibifu katika Senta, sehemu kubwa ilibaki bila kuharibiwa na kimbunga and picha za rangi ya ukutani zilibaki zikionekana. Ni mwezi sasa tangu kimbunga, mkusanyiko wa sala ulifanywa kila asubuhi katika Senta ya Kibahá’í na wale waliokua wakijihifadhi hapo, na yeyote aliyependa. Mkusanyiko wa jumuia yote wa sala, uliokua wazi kwa watu wote, ulipangwa katika mwisho wa wiki na vijana ambao walikua wakisaidia kusafisha barabara na kuleta misaada kisiwani wakati wakijiandaa na matukio ya miaka mia mbili.