Malaysia

Maonesho ya Jenjarom yakikaribisha uchunguzi wa ujumbe wa Bahaú’llah

Maonesho yakiitwa "Kujenga Jamii Bora" kwenye kijiji cha Jenjarom (Nje ya Kuala Lumpur) yaliandaliwa na jamii ya ki- Bahá’í kama mojawapo ya ufikiaji katika kipindi hiki cha sherehe za miaka mia mbili. Eneo hilo ni makao makuu ya kujifunza katika kijiji. Maonesho yalionesha umuhimu wa elimu ya kiroho na ya jamii zilizoungana. Wiki chache zilizopita, viongozi wa vijiji, walimu, wazazi na watoto, walitembelea maonesho, ambayo yalisisimua maongezi mazuri na maangalio chanya. Kulikuwepo pia vyombo vya habari.