Katika vitongoji vya Toronto, sherehe za miaka mia mbili zilifanyika katika nyumba, senta za jumuia, hifadhi na majukwaa ya mashuleni. Jamii zilishirikiana zenyewe kwa sala, maandiko na hadithi kutoka maisha ya Bahá’u’lláh.
Vijana waliandaa mabango na maonesho yanayoonesha matukio muhimu katika maisha ya Bahá’u’lláh. Watoto walishiriki na jamii hadithi na nyimbo. Katika moja ya kitongoji cha Toronto, kikundi cha vijana wadogo walitengeneza taa za makaratasi kwa muda wa siku tatu kwa ajili ya kila familia - wakionesha mafano wa mwanga wa mafundisho ya Bahá’u’lláh na jinsi yalivyovigusa vitongoji.