Kyrgyzstan

Sherehe za Bishkek zavutia watu 300

Bishkek- mji mkuu wa Kyrgyzstan - ni mji wenye mitaa mikubwa, ikizungukwa na milima iliyofunikwa kwa theluji ya Ala-Too. Kwa miezi mingi, jamii ya Wabahá’í walifanya kazi ya kuwaalika marafiki wengi, familia, majirani na wafanyakazi wenzao, kwenye sherehe. Masaa machache, wageni 300, waliokuwa wakitaka kujifunza kuhusu maisha na mafundisho ya Bahá'u'lláh- waliungana na marafiki zao kwenye sehemu ya wazi ya ukumbi wa kati karibu na Chuo cha Marekani cha Asia ya kati. Ratiba ilijumuisha kutazama filamu ya *Mwanga wa Dunia* na maonesho ya sanaa ya dansi iliyoonesha umoja wa dini. Baada ya sherehe, baadhi ya wageni walihamasika kutokana na walichojifunza kuhusu maisha ya Bahá'u'lláh na waliungana na marafiki zao majumbani kwao kuendelea na mazungumzo.