The Universal House of Justice

OKTOBA 2017

Kwa wote wanaousherehekea Utukufu wa Mungu

Marafiki wapendwa sana,

Tunasisitiza ukweli huu ufaao: kwamba watu wa dunia daima wamekuwa wakikumbukwa na Mungu wao.katika kila zama za historia, kwamba Uhalisi usiojulikana umefungua milango ya neema kwa ulimwengu kwa kumtuma Mjumbe akiwajibika kutoa kichocheo cha kimaadili na kiroho ambacho binadamu hukihitaji ili kushirikiana na kupiga hatua. Mengi ya majina ya Miangaza hii mikuu kwa binadamu imepotea. Lakini baadhi hung’aa kutoka kumbukumbu za kihistoria kama zenye fikra za kimapinduzi, zilizofungua ghala za ujuzi, na kuvuvia uibukaji wa ustaarabu, na majina Yao yanaendelea kuheshimika na kusifika. Kila mmoja wa hawa wenye maono ya mbali kiroho na kijamii, vioo visivyo na mawaa vya njema, walileta mafundisho na kweli ambazo zilijibu mahitaji ya haraka ya zama husika. Kwa kuwa ulimwengu hivi sasa unakabiliwa na changamoto zake zinazoshinikiza kabisa hata hivyo, sisi tunampokea kwa shangwe Baha’u’lláh, aliyezaliwa miaka mia mbili iliyopita, kama Yule mtu – kwa kweli, kama Yeye Ambaye mafundisho Yake yataleta kile kipindi ambacho kiliahidiwa tangu muda mrefu ambapo wanadamu wote wataishi bega kwa bega kwa amani na umoja.

Tangu ujana Wake wa mwanzoni, Bahá’u’lláh alifikiriwa na wale waliomfahamu kama abebaye hatma ya fikra za moyoni. Akiwa amebarikiwa na tabia takatifu na hekima isiyo ya kawaida, Yeye alionekana kuguswa na nuru njema ya mbinguni. Hata hivyo Yeye alilazimishwa kustahimili miaka arobaini ya mateso, ikiwa ni pamoja na uhamisho mfululizo na vifungo kwa amri ya wafalme wawili wadhalimu, kampeni za kulikashfu jina Lake na kuwalaani wafuasi Wake, vurugu juu ya Utu Wake, majaribio ya aibu ya kutoa uhai Wake – yote haya, kutokana na upendo usio na mipaka kwa wanadamu, Yeye kwa ridhaa aliyavumilia, kwa wangavu na ustahimilifu, na kwa huruma kwa ajili ya watesi Wake. Hata unyang’anywaji wa mali Zake zote za kidunia haukumsumbua hata kidogo. Mtu angeweza kujiuliza kwa nini Yeye Ambaye upendo Wake kwa wengine ulikuwa mkamilifu mno angeweza kufanywa mlengwa wa chuki kuu kama hiyo, ukizingatia kwamba hapo awali Alikuwa anasifika na wote kwa heshima na haiba, umaarufu wa wema na akili Yake ya juu, na alikuwa amekataa masuala yoyote ya uwezo wa kisiasa. Kwa yeyote ambaye ana uzoefu na ruwaza ya historia, sababu ya mateso Yake, bila shaka, ni dhahiri. Utokezaji wa Nabii ulimwenguni daima umesababisha upinzani mkali sana kutoka kwa wenye uwezo. Lakini mwanga wa ukweli hautazimwa. Na hivyo, katika maisha ya Viumbe hawa wa juu kabisa mtu huona dhabihu, ushujaa na, lolote liwalo, matendo ambayo huonesha mfano wa maneno Yao. Jambo hilo hilo lipo dhahiri katika kila hatua ya maisha ya Bahá’u’lláh. Licha ya kila shida, Yeye kamwe hakuzibwa mdomo, na maneno Yake yaliendelea kubaki na uwezo wake ushurutishao vyote – maneno yaliyonenwa kwa sauti ya umaizi, yakibaini magonjwa ya ulimwengu na kuamuru tiba; maneno yaliyobeba uzito wa haki, maonyo kwa wafale na watawala kuhusu nguvu ambayo hatimaye ingewafagilia mbali kutoka kwenye viti vyao vya enzi; maneno ambayo huiacha roho ya mtu ikiinuliwa, yenye kicho na yabadilishayo, yakidhamiria kujiachilia yenyewe huru kutoka miiba na mikwamba ya ubinafsi; na maneno ambayo yapo dhahiri, yenye kuzuia na yenye mkazo: "Jambo hili halitoki Kwangu, bali latoka kwa Mungu." Je, mtu asingeweza kujiuliza, katika kufikiria maisha kama hayo: kama hili halitoki kwa Mungu, ni kitu gani kingeonesha hilo?

Waelimishaji wakamilifu Ambao, katika kipindi chote cha historia, wameleta mwanga ulimwenguni, wameacha urithi wa maneno matakatifu. Ndani ya maneno ambayo hutiririka kama mto kutoka kalamu ya Bahá’u’lláh ni tunu za mlolongo mkubwa mno na tabia bora kupita kiasi. Ni nadra, mtu ambaye hukutana na Ufunuo Wake hujibu kwanza sala za uzuri upitao vyote ambao hukidhi shauku ya roho istahiliyo kumuabudu Muumba wake. Ndani kabisa ya bahari ya maneno Yake ziligunduliwa sheria na maadili muhimu kuiachilia roho ya binadamu kutoka udhalimu wa tamaa za kidunia zisizostahili mwito wake wa kweli. Hapa, vile vile, hupatikana mawazo bora kabisa ambayo katika mwanga wake wazazi huwalea watoto si kama watakavyo wao wenyewe tu, bali kwa matarajio yaliyotukuka zaidi.

Pia kuna maelezo ambayo huonesha mkono wa Mungu ufanyao kazi katika historia ya safari ipindayo ya binadamu kupitia hatua za kabila na taifa kuelekea aina za juu zaidi za umoja. Dini anuai za ulimwengu huoneshwa kuwa vielelezo vya ukweli mmoja wa kimsingi, zikihusiana moja kwa nyingine kwa asili moja, na pia kwa kusudi moja: kubadilisha maisha ya ndani ya binadamu na hali za nje. Mafundisho ya Bahá’u’lláh hushuhudia kwenye ubora wa roho ya mwanadamu. Jamii aliyoibuni ni ile istahiliyo ule ubora na iliyowekwa juu ya kanuni ambazo huilinda na kuiimarisha. Umoja wa familia ya binadamu Yeye huuweka kwenye msingi wa maisha ya pamoja; usawa wa wanawake na wanaume Yeye huusisitiza bila mjadala. Yeye anapatanisha nguvu zionekanazo kugongana za wakati wetu – sayansi na dini, umoja na anuai, uhuru na utaratibu, haki za mtu mmoja mmoja na wajibu wa kijamii. Na miongoni mwa zawadi Yake kuu kabisa ni haki, zinazodhihirishwa katika asasi ambazo haja yake kuu kabisa ni upigaji hatua na maendeleo ya watu wote. Katika maneno Yake mwenyewe, Yeye "amefutilia mbali kutoka katika kurasa za Kitabu Kitakatifu cha Mungu chochote ambacho kimekuwa chanzo cha ugomvi, cha husuda na ubaya miongoni mwa watoto wa watu" na, wakati huo huo, "aliweka mahitaji ya lazima ya upatano, ya uelewa, ya umoja kamili na wa kudumu." Je, mtu hawezi kujiuliza, ni lipi lingekuwa jibu linalostahili kwa zawadi kama hizo?

"Ni wajibu wa kila mtafutaji kujishughulisha mwenyewe na kujitahidi kuzifikia fukwe za bahari hii,"

Bahá’u’lláh hueleza. Mafundisho ya kiroho yaliyoletwa na Wajumbe waliofuatana katika zama zote huonekana katika mifumo ya dini kwamba, baada ya muda yameingizwa masuala ya kitamaduni na kuelemewa na mafundisho yaliyotungwa na wanadamu. Lakini yaangalie haya kwa wakati uliopita na inakuwa wazi kwamba mafundisho halisi ni chanzo cha tunu za jumla ambazo kupitia kwazo watu wa anuai mbalimbali wamepata chanzo kimoja na ambayo yamebumba fikra za kimaadili za ufahamu wa binadamu. Katika jamii ya sasa, hadhi ya dini imeteseka sana, na inaeleweka kwa nini. Kama, katika jina la dini, chuki na ugomvi vinaendelezwa, ni bora kutokuwa nayo. Hata hivyo, dini ya kweli inaweza kujulikana kwa matunda yake – uwezo wake wa kuvuvia, kubadilisha, kuunganisha, kudumisha amani na ustawi. Inapatana na fikra ya kimantiki. Na ni lazima kwa maendeleo ya kijamii. Imani ya Bahá’u’lláh hujenga ndani ya mtu binafsi na jumuiya nidhamu ya kutenda kwa mujibu wa tafakari, na kwa njia hii pole pole umaizi hujikusanya kuhusu njia zifaazo za kutenda kazi kwa ajili ya uboreshaji wa jamii. Majaribio ya kuleta mabadiliko ya kijamii kupitia njama za kisiasa, uchochezi wa uasi, ukashfu wa makundi maalum, au ugomvi wa moja kwa moja yanalaaniwa na Bahá’u’lláh, kwani yanaendeleza tu kujirudia-rudia kwa misukosuko wakati ufumbuzi wa kudumu unaendelea kuepukwa kwa hila. Yeye ameleta vyombo vya aina tofauti sana. Hutoa wito kwa matendo mema, maneno mema, na mwendendo mnyoofu; Huagiza huduma kwa wengine na utendaji shirikishi. Na kwa kazi ya ujenzi wa ustaarabu wa ulimwengu wenye misingi ya mafundisho matakatifu, Anamualika kila mwanajamii ya binadamu. Je, mtu asingeweza kuuliza, katika kutafakari upana wa maono Yake, ni juu ya msingi gani jamii ya binadamu kiuhalisia itajenga matumaini kwa ajili ya siku zijazo, kama siyo huu?

Katika kila nchi, wale ambao wamevutiwa na ujumbe wa Bahá’u’lláh na wamejidhatiti kwa muono Wake wanajifunza kimpangilio jinsi ya kufanikisha mafundisho Yake. Makundi ya vijana daima yanaendelea kutambua zaidi juu ya utambulisho wao wa kiroho na wanaelekeza nguvu zao kwenye maendeleo ya jamii zao. Watu wenye mitazamo tofauti wanatambua jinsi ya kutumia ushauriano na utafutaji wa pamoja wa ufumbuzi badala ya mabishano na ulazimishaji wa mamlaka. Kutoka kila mbari, dini, taifa, na tabaka, roho zinaunganika kuzungukia muono wa wanadamu kama wamoja na dunia kama nchi moja. Wengi ambao wameteseka kwa muda mrefu wanapata fursa kutoa sauti yao na kuwa waongozaji wa maendeleo yao wenyewe, wabunifu na wanyumbulifu. Kutoka vijiji, ujirani, miji na majiji zinainuka asasi jumuiya, na watu binafsi waliojidhatiti kufanyakazi pamoja kwa ajili ya uibukaji wa ulimwengu uliounganika na kustawi ambao kwa kweli unaweza kustahili kuitwa ufalme wa Mungu duniani. Kwenye maadhimisho haya ya miaka mia mbili ya kujitokeza kwa Bahá’u’lláh, wale wengi ambao ni sehemu ya shughuli hii wanawafikia wale wanaowazunguka kwa mwaliko wa rahisi: tumia fursa hii kutafuta Yeye alikuwa nani na nini anachowakilisha. Ijaribu tiba Aliyoamuru. Ujio Wake hutoa ushuhuda wa uhakika kwamba mbari ya binadamu, iliyotishiwa na mateso lukuki, haijasahaulika. Pale ambapo watu wengi mno wenye nia njema kote ulimwenguni kwa muda mrefu wamemsihi Mungu awape jibu kwa ajili ya matatizo ambayo yanayowakabili katika nchi zao za kuzaliwa, je, inashangaza kwamba Yeye Amewajibu sala zao?

[signed: The Universal House of Justice]